Jumatatu, Januari 06, 2014

WATANZANIA WAMSHANGAA RAY C BAADA YA KUMKANDIA JACK PATRICK

Kufuatia sakata la Jack, hivi karibuni, staa wa muziki wa kizazi kipya Tanzania, Rehema Chalamila ‘Ray C’ aliingiza kwenye mtandao wake wa kijamii akitoa maoni kwamba Jack apewe adhabu kali zaidi ya kifungo (pengine kunyongwa) hali iliyowashangaza wengi waliotembelea mtandao huo.
Baadhi ya watu waliozungumza na Uwazi baada ya staa huyo kuingiza mawazo yake walimshutumu wakisema alitakiwa kutafakari upya.
“Yule dada (Ray C) hakutakiwa kumtakia mwenzake mabaya zaidi, kama yeye aliathirika na madawa na amepona anatakiwa kuwa balozi kwa wengine na si kuwahukumu wenzake,” alisema Joan Mushi, mkazi wa Sinza ‘E’ jijini Dar.
WAZIRI MEMBE VIPI?
Juzi, Fichuo Tz lilimtafuta Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Kamillius Membe ili azungumze lolote kuhusu sakata la Jack Patrick lakini hakupatikana badala  yake naibu wake, Mahadhi Maalim alisema taarifa za Jack kukamatwa amezisikia  kupitia vyombo vya habari na hana habari kiundani ila bosi wake anaweza kuwa na maelezo zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni