Jumapili, Aprili 20, 2014

IFAHAMU NAMBA YAKO YA BAHATI NA JINSI YA KUITUMIA UFANIKIWE

Katika Ulimwengu wa sasa namba ni sehemu ya maisha yako , unaitumia kila siku ukitaka usitake , kwa kuwasiliana na binaadamu wenzio, kuangalia muda, kuhesabu Pesa na kadhalika. Kila mtu katika dunia hii anataka kupata mafanikoi, na wengi wenu mnataka kujua namba zenu za Bahati au namba yako muhimu na mamba ya kuitumia katika kuweza kupata mafanikio katika maisha yako aidha ya kimapenzi kikazi kibiashara au kiuchumi.

Watu wote wanataka kutumia namba zao za bahati katika kufanya mambo muhimu au maamuzi muhimu, kama kuanzisha biashara, kuoa, kuanza Ujenzi, kujifurahisha na kufanya usaili au kuanzisha shughuli ambazo zitakuwa na mafanikio katika maisha yao,
Jambo la kwanza unalotakiwa kujua ni kwamba namba yako ya bahati ni ipi? La pili ni namna gani au ni vipi unaweza kuongeza nguvu ya hiyo namba yako ya bahati ilikupata unachokitaka hasa unapokuwa tayari umeshaigundua.

Namba yako ya Bahati au namba yako muhimu hupatikana kutokana na TAREHE YAKO YA KUZALIWA, ni nyepesi tu, utafiti uliofanyika miaka Elfu nyingi iliyopita kwa elimu ya nambari au Numerology umethibitisha kwamba siku uliyozaliwa ndio siku yako ya bahati na ni siku muhimu sana kwako na katika maisha yako. Mfano chukulia mtua aliyezaliwa tarehe 14 ya mwezi wowote namba yake ya bahati itakuwa 1 + 4 = 5 na Yule aliyezaliwa tarehe 7 namba yake ya bahati itakuwa namba 7.

Sasa kwa vile ushajua namba yak o ya bahati jambo la pili ni namna gani unaweza kuongeza uwezo wa namba hiyo ili ikusaidie katika kufanikisha mambo yako.

Kwanza kabisa unatakiwa uwe unaijua kichwani na kuifikiria, uwe unajua hiyo namba yako kila mwezi huwa inakuwa ni siku gani kama namba yako ya bahati ni 5 tarehe yyoyte ya mwezi ambayo ukijumlisha unapata 5 ni siku nzuri kwako, mfano tarehe 14 na 23,
Wale waliozaliwa tehe 3 siku nzuri itakuwa hiyo ya tarehe 3, 12 na tarehe 30 katika tarehe hizo fanya jambo lolote utafanikiwa, ukifanya maamuzi yatakuwa mazuri, ukifanya mtihani au usaili utafanikiwa, ukianza biashara utapata mafanikio na lolote utakalofanya katika tarehe hizo litakwenda vizuri sana.

Maelezo haya au sheria hii inatumika kwa namba zote isipokuwa 4 na 8 kwa sababu namba hizi hazitakiwi kuvunjwa zinabaki kama zilivyo kwa sababu kuzivunja hizi kunaleta bala na mikosi.
Wale waliozaliwa katika tarehe hizi za 4 na 8 huwa katika maisha yao wanakumbana sana na misukosuko, mikwamo na matatizo katika maisha yao kuliko namba nyingine yoyote.
Kwa hiyo kama umezaliwa tarehe 4 unatakiwa uchague namba 1 kama nambo yako ya bahati na mambo yako unayafanya katika tarehe za namba hiyo kwa mfano tarehe 1, 10, 19, 28….
Wale wa namba 8 wachague namba 3 kama nambo yako ya bahati na mambo yako unayafanya katika tarehe za namba hiyo kwa mfano tarehe 3, 12, 21, 30…. Ni sikuambazo unaweza kufanya mipango yako Muhimu.

Unapoanza kutumia sheria ya kutumia namba yako ya bahati na namba yako ni muhimu sana kuzingatia uwezo na namna ya kuongeza uwezo wake hiyo namba utaanza kuona mafanikio katika mambo yako binafsi au biashara zako.

Mabadiliko yanaweza yasiwe kwa siku moja au haraka kama unavyotazamia lakini utaweza kuona mabadiliko katika kipindi cha miezi mitatu. inatengemea ni namna gani unaitumia hiyo namba yako ya bahati.

Kwa wale wasiojua tarehe zao za kuzaliwa namba zao za Bahati wanaweza kuzijua kwa herfi ya mwanzo ya jina lako maarufu au ulilopewa wakati unazaliwa kama ifuatavyo

A J S namba 1, B K T Namba 2, C L U Namba 3, D M V Namba 4, E N W Namba 5 F O X Namba 6, G P Y Namba 7, H Q Z Namba 8, na I R Namba 9

0 comments:

Chapisha Maoni