Jumatatu, Januari 06, 2014

KESI YA JACK PATRICK KUSIKILIZWA 2016 CHINA

Mrembo huyo alikamatwa Desemba 19, mwaka jana katika Uwanja wa Ndege wa Macau akitokea Bangkok, Thailand akiwa na kete 57 (kilo 1.1) za unga aina ya heroin tumboni zikiwa na thamani ya shilingi milioni 300. 
Jack Patrick
TAARIFA MBICHI
Taarifa mbichi kabisa zinadai kwamba, Jack amepewa mwaka mmoja na nusu (siku 447) ajifunze lugha inayozungumzwa na watu wa Macau (Kireno) ambayo ndiyo itakayotumika mahakamani wakati kesi yake itakapoanza kuunguruma.
Sheria ya kisiwa hicho inasema kuwa mshitakiwa yeyote atakayefikishwa kortini, kesi yake haitasikilizwa mpaka majaji wakubali kwamba anajua lugha hiyo na si kinyume na hapo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, mwalimu maalum anayejua Lugha za Kiingereza na Kireno ndiye atakayemfundisha Jack mpaka atakapojua.

Dawa za kulevya alizokuwa amezubeba Jack Patrick tumboni
AKIJUA MAPEMA ITAMSAIDIA
Habari za ndani kutoka vyanzo vya uhakika nchini humo zinasema kwamba, kama Jack angekuwa anakijua Kireno angepandishwa kizimbani mara baada ya upelelezi kukamilika, Machi mwaka huu.
KIFUNGO CHA CHINI MIAKA 16
Habari nyingine mpya kutoka Macau zinasema kuwa, sheria za eneo hilo kuhusu makosa ya kukutwa na madawa ya kulevya, mtuhumiwa akitiwa hatiani kifungo cha chini ni miaka 16 kulingana na mwenendo wa kesi.
SERIKALI YA TANZANIA YASUBIRI ORODHA…
Juzi, Uwazi liliwasiliana kwa simu ya mkononi na Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa na kumuuliza kuhusu nini kinaendelea kati ya serikali na utawala wa Macau kufuatia Mtanzania, Jack Patrick kunaswa na unga nchini humo.
Nzowa: “Aaah! Sisi tumetuma maswali yetu kule (Macau) kupitia Polisi wa Kimataifa (Interpol), tumetaka kujua kama huyo binti (Jack) amewataja vigogo waliomtuma ni majina gani wanayo.
“Ndiyo tunasubiri majibu yao ili tujue nini kinaendelea kule. Kama aliwataja watu tutaanza kuwafuatilia mara moja maana lazima kuna vigogo nyuma yake.”

0 comments:

Chapisha Maoni