Alhamisi, Agosti 28, 2014

SEIRRA LIONE NA MGOGORO WA CHAKULA

Shirika la Kilimo na Chakula Duniani (FAO) limeonya juu ya mgogoro wa chakula unaoikabili nchi Sierra Leone. Ripoti iliyotolewa na shirika imeeleza kuwa kupandisha bei za bidhaa nchini humo kumewafanya wananchi wengi kukabiliwa na matatizo ya kujidhaminia mahitaji ya chakula cha kila siku ndani ya nchi hiyo. 
Katika ripoti hiyo ya FAO imeashiria maambukizi ya virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola nchini humo na kuzitaja pia siasa za serikali ya Freetown kuwa chanzo cha ongezeko la mfumuko wa bei. Shirika hilo la chakula na kilimo limeitaja marufuku iliyowekwa na serikali kwa lengo la kuzuia maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo kuwa iliwafanya wakulima washindwe kuendelea na shughuli zao. 
Awali Wizara ya Kilimo ya Sierra Leone, ilikuwa imetangaza kuwa, tangu mwezi Mei mwaka huu ambapo kuliibuka ugonjwa wa Ebola nchini humo, wakulima wameshindwa kuvuna mazao yao. 
Kwengineko mkuu wa Shirikisho la Kitaifa la Wakulima nchini Sierra Leone, ameonyesha masikitiko yake kutokana na hasara kubwa ya mazao ya kilimo iliyotokana na uharibifu wa mazao ya kilimo nchini. 
Watu 910 wameshapoteza maisha yao kutokana na ugonjwa huo wa Ebola nchini Sierra Leone.

0 comments:

Chapisha Maoni