Alhamisi, Agosti 28, 2014

HOFU YATANDA MANCHESTER UNITED

Kuna mawazo yameanza kutanda katika fikra za wadau wa soka kuhusu mwenendo wa Manchester United na kuporomoka kwa kasi kwa klabu hiyo katika misimu ya hivi karibuni.
United wameanza msimu huu vibaya chini ya uangalizi wa meneja wao Louis van Gaal, wakishindwa kupata ushindi katika michezo miwili ya Premier League dhidi ya Swansea na Sunderland kabla kuaibishwa kwa bao 4-0 dhidi ya MK Dons katika kombe la Capital One.
Paul Scholes amekiri kupata uoga juu ya mwenendo wa klabu hiyo ambayo aliitumikia vizuri. Inagwa mchezaji mwingine nguli wa klabu hiyo Andy Cole, bado anaamini kwamba klabu hiyo itaibuka tena na kua na makali yake ya kawaida.
Waliokua na mashaka kwani Liverpool kwa wakati huo ikiwa inatawala vilivyo Uingereza na Ulaya miaka ya 80, iliporomoka hasa katika soka la nyumbani na kufikia kukumbukwa kwa historia yao tu. Miaka 20 sasa ndio Liverpool wameanza kuonesha dalili za kujizatiti ingawa ushindani ni mkubwa na hakuna uhakika kama watafanikiwa kujisimika tena kama klabu inayotwaa vikombe kila mwaka Uingereza.
Kama hilo liliweza kuwatokea Liverpool dalili zile zile ndizo zinaonekana kwa United sasa, kwani gharama za kurudi tena kileleni hua ni kubwa na muda ni mrefu sana(Liverpool miaka 20).
Nini maoni yako: United wataibuka tena ama unadhani zama zao ndio zinamalizikia malizikia?

0 comments:

Chapisha Maoni