Alhamisi, Agosti 28, 2014

REKODI MPYA ILIYOVUNJWA NA WAKIMBIZI WA AFRIKA

Takribani wahamiaji 1,900 wamepoteza maisha yao kwenye bahari ya Mediterenia mwaka huu wakijaribu kuvuka kuingia Ulaya kutoka Afrika Kaskazini, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaowahudumia Wakimbizi (UNHCR) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).
Idadi hiyo inavuka ile ya watu zaidi ya 700 iliyorekodiwa mwaka 2013 na 500 mwaka 2012. Mathalani UNHCR inasema katika siku nne zilizopita watu wapatao 300 wamefariki dunia katika majanga matatu mbali mbali ya mashuani kwenye bahari hiyo ya Mediterenia.
Matukio hayo yalihusisha boti tatu za kiasili zikitoka Libya huku ikisema kuwa machafuko ya sasa na kukosekana kwa utulivu Libya ndio vinachochea ongezeko la biashara haramu ya usafirishaji binadamu, halikadhalika wahamiaji nchini Libya kutafuta njia yoyote ya kutoroka.
Nchi nyingine ni Eritrea na Syria ambazo zina idadi kubwa ya wahamiaji wanaowasili Italia kwa njia ya bahari.

0 comments:

Chapisha Maoni