Alhamisi, Agosti 28, 2014

MWANAMKE AKAMATWA NA GONGO MBEYA

Mtu mmoja aitwaye Christina Mgala (41) mkazi wa Itiji anashikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Mbeya akiwa na pombe haramu ya moshi ujazo wa robo lita.
Mtuhumiwa alikamatwa jana majira ya saa 11:50 jioni huko Majengo, kata ya Itiji, tarafa ya Sisimba, jiji na mkoa wa Mbeya. Mtuhumiwa ni mtumiaji wa pombe hiyo, taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi Ahmed Z. Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia pombe haramu ya moshi kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

0 comments:

Chapisha Maoni