HABARI KWA WAKATI KUTOKA HAPA

Tunakuhakikishia kupata habari zote zilizo muhimu kutoka ulimwenguni kote kwa wakati, unaweza kusubscribe mtandao wetu na ukawa unapokea habari zote katika email yako punde tu tuchapishapo machapisho yetu. Jiunge na mitandao yetu ya Facebook na Twitter kutupata kirahisi.

Jumanne, Machi 13, 2018

GARI LA MIZIGO LACHOMWA MOTO BAADA YA KUMGONGA MUUGUZI NA KUMSABABISHIA KIFO

Kundi la watu limechoma gari la mizigo baada ya dereva wake kumgonga na kufa papo hapo muuguzi wa Zahanati ya Kaseme wilayani Geita.Tukio hilo limetokea Jana usiku katika Kijiji cha Kaseme wakati marehemu huyo akiwa katika Bodaboda pamoja na watoto wake wawili, mmoja amefahamika kwa jina Paulo Tarafa mwenye miaka 3 na mwingine mchanga wa miezi miwili ambao wao wamenusurika na kifo hicho.Mashuhuda wa tukio hilo wamesema lori hilo...

NJIA 6 ZA KUJIKINGA NA RADI

Tafuta hifadhi pahali ambapo kuna jumba kubwa au ndani ya gari. Kukiwa na jumba ambalo lina kifaa cha kukinga dhidi ya radi, utakuwa salama zaidi. Usiwe katika maeneo ya wazi, au kwenye mlima ulio wazi. Iwapo utakosa pahala pa kujikinga mvua, punguza uwezekano wako wa kupigwa kwa kujikunyata na kujifanya mdogo zaidi. Unaweza kuchutama, kuweka mikono yako kwenye magoti na kufichwa kichwa chako ndani. Usijikinge mvua chini ya miti. Iwapo...

Jumatatu, Machi 05, 2018

75% YA WANAOACHA KAZI HUACHA SABABU YA 'MABOSS' WAO

Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na watafiti kutoka shirika la kazi ulimwenguni ILO imebainika kuwa asilimia kubwa ya waajiriwa wanaoziacha kazi zao walikoajiriwa huacha kazi huwa sababu halisi ni 'maboss' wao. Tunaambiwa kuwa 75% ya waajiriwa anaojiuzulu nafasi zao katika ajira ni wale wenye matatizo mbalimbali na viongozi wao kwenye mashirika, na 25% inayosalia pekee ni wale wanaoacha kazi zao kwa sababu nyinginezo. Mashirika mengi kutokana...

Jumapili, Machi 04, 2018

AJALI NYINGINE MBILI MBAYA ZA MABASI ZILIZOTOKEA LEO NA KUUA. (+PICHA)

Baada ya taarifa tuliyokupatia jana kuhusu ajali mbili za mabasi ya abiria zilizotokea katika mikoa ya Tanga na Songwe mabasi ya Lim Safari na New Force yakihusika na kisababisha mauti kwa mtu mmoja, leo tena jumapili machi 4, 2018 ajali mbili zimetokea katika mikoa ya Morogoro na Iringa na kusababisha vifo kwa watu 5.       Katika ajali iliyotokea mkoani Morogoro  watu 5 wamefariki na wengine 9 kujeruhiwa baada ya...

Jumamosi, Machi 03, 2018

TRENI ILIYOPATA AJALI UVINZA ILISABABISHWA NA KICHWA 'KILICHOOKOTWA' BANDARINI!!!???

Mambo yameanza kuibuka baada ya treni ya kubeba abiria iliyokuwa safarini kutoka Dodoma kwenda Kigoma kupitia Tabora kupata ajali katika eneo la kijiji cha Mpeta, wilayani Uvinza kaskazini magharibi mwa Tanzania, taarifa zinasema. Ajali hiyo ilisababishwa na kichwa cha treni kuacha njia na mabehewa mawili kuanguka. Kaimu meneja wa wamawasiliano wa Shirika la Reli la Tanzania (TRL) Mohamed Mapondela alithibitisha kwamba watu watatu wamejeruhiwa. Utakumbuka...

AJALI MBILI ZA MABASI LEO SONGWE NA TANGA

Ajali mbili zimetokea leo katika mikoa ya Songwe na Tanga na kusababisha kifo ch mtu mmoja na majeruhi kadhaa. Huko mkoani Songwe asubuhi ya leo imetokea ajali iliyohusisha magari mawili, basi la abiria kutoka kampuni ya New Force na gari dogo aina ya Altezza ambapo sababu ya ajali hiyo ikitajwa kuwa ni uzembe wa dereva wa gari hilo dogo aliyehama upande na kuligonga basi hilo akiwa mwendo kasi. Katika ajali hiyo dereva wa Altezza amefariki...

Jumanne, Februari 27, 2018

UNAAMBIWA KUOGELEA BAHARINI KUNASABABISHA MAGONJWA!!!

Kuogelea baharini kunaongeza kwa kiwango kikubwa kuwa na matatizo ya tumbo , kuumwa na masikio na magonjwa mengine , watafiti wamebaini. Chuo kikuu cha matibabu cha Exeter na kituo cha Ekolojia na maji ardhini kilifanya utafiti huo. Ulibaini kwamba uwezo wa muogeleaji wa baharini kuwa na tatizo la masikio uko juu ikilinganishwa na waogeleaji wa maeneo mengine huku matatizo ya tumbo pia yakipanda hadi asilimia 29. Mbali na kuogelea, hatari...

Jumatatu, Februari 26, 2018

NUKUU 6 ZA TUNDU LISSU BAADA YA HUKUMU YA JOSEPH MBILINYI (SUGU) NA EMMANUEL MASONGA

Jana mbunge wa Mbeya mjini Joseph Mbilinyi, Sugu (Chadema)  na mwenzake Katibu wa Chadema Kanda ya Nyasa Emmanuel Masonga walihukumiwa kifungo jela miezi mitano kila mmoja. Wawili hao walikuwa wameshtakiwa kwa kosa la kutumia lugha ya dhihaka dhidi ya Rais John Magufuli. Wanadaiwa kutenda kosa hilo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika mwezi Desemba 31, 2017 jijini Mbeya. Hukumu dhidi yao imetolewa na Mahakama ya hakimu mkazi jijini...

UTAMADUNI WA KUCHEZA UTUPU MSIBANI CHINA UNAZIDI KUSHIKA KASI

Muziki unacheza kwa sauti, wacheza utupu wakicheza densi na umati ukishangilia. Katika sehemu zingine huko China hili ndilo unaweza kuliona wakati wa mazishi.Mapema mwaka huu, China alianza tena kuwakamata wacheza utupu wanaocheza densi kwenye mazishi, harusi na kwenye mahekalu.Hio sio mara ya kwanza mamlaka zimejaribu kuzuia tabia hizo lakini bado hazijanafikiwa Mbona watu huwaajiri wacheza utupu? Wacheza utupu hutumiwa kuwavutia watu wnaaohudhuria...

Jumapili, Februari 25, 2018

WATU WANAOSHEREHEKEA SIKUKUU YA CHRISTMAS MWEZI FEBRUARI

Wanakijiji wanasema kuwa utamaduni huu ambao ulianza enzi za utumwa wakati mababu zao walipozuiwa kusherehekea Krismasi tarehe 24 Desemba kama ilivyo kawaida kwa madhehebu mengi ya Kikristo. Badala yake waliamua kuchagua katikati mwa mwezi wa Februari na utamaduni huu umeendelea tangu wakati huo. Fataki, muziki na densi huwa sehemu ya sherehe hizo za kuvutia. "Watu waliotufanya watumwa walisherehekea Krismas Desemba na hatukuruhusiwa kuwa...

Page 1 of 1619123...1619Next »Last