Jumapili, Februari 19, 2017

KEMIKALI INAYOWEZA KUUMBA KIUMBE HAI HII HAPA

Kwenye gazeti jipya la Sayansi la Marekani, wanasayansi wamesema chombo cha uchunguzi wa sayari ndogo cha "Dawn" kilichorushwa na idara ya safari ya anga ya juu ya Marekani NASA kimegundua kemikali ya kikaboni inayoweza kuunda viumbe karibu na shimo lililosababishwa na mgongano wa vimondo lenye kipenyo cha kilomita 50 lililoko kaskazini mwa sayari kibete ya Ceres. 
Muundo wa molekuli za kemikali hiyo bado haujathibitishwa, lakini kemikali hii inafanana na kemikali inayounda mwamba wa lami.
Mtafiti mwandamizi wa taasisi ya kusini magharibi ya Marekani Dr. Simone Marchi amesema ingawa karibu na eneo hili kuna mashimo mengi yaliyosababishwa na mgongano wa vimondo, lakini kemikali hiyo haikupelekwa kwenye sayari hiyo na vimondo.
Mwanasayansi wa sayari wa kituo cha unajimu cha Ulaya Dr. Michael Kuppers ambaye pia ametoa makala kwenye gazeti la sayansi akisema joto lililokuwepo wakati sayari ya Ceres ilipoundwa huenda bado linahifadhiwa ndani ya sayari hiyo. 
Wanasayansi wanaona kuna barafu nyingi kwenye sayari hii, na chini ya barafu huenda kuna bahari, ambayo inatoa uwezekano wa kutokea kwa viumbe.

0 comments:

Chapisha Maoni