Jumapili, Februari 19, 2017

ALIYEFANYIWA UPASUAJI WA AJABU AJISTAAJABU

Tarehe 16 mwezi Juni 2016 Andy Sandness alisafirishwa na kuingizwa ndani ya chumba cha upasuaji katika kliniki ya Mayo huko Rochester Minnesota ili kufanyiwa upasuaji usio wa kawaida duniani.
Wiki tatu baadaye alijiangalia kwenye kioo asijue ni nini angeona.
Sura alioona katika kioo haikuwa yake bali ya mtu mwengine ,pua, mashavu, mdomo, taya kidevu na hata meno ya mtu aliyemfadhili kiungo hicho Calen Ross.
Bwana Sandness kutoka eneo la Wyoming aliwachwa na uso uliokuwa umeharibiwa kabisa baada ya jaribio la kujiua 2006.
Mfadhili wake, Bwana Ross ambaye aliishi Minnesota hakupona alipojipiga risasi mwaka 2016 na kumwacha nyuma mjane aliyekuwa na mimba Lily asijue la kufanya.
Alitaka kutekeleza wazo la mumewe la kufadhili viungo lakini aliogopa mtu mwengine kuchukua uso wake.
Lakini alikubali baada ya kuhakikishiwa kwamba bwana Sandness alikuwa na macho na paji lake la uso na hatofanana na marehemu mumewe.

0 comments:

Chapisha Maoni