Polisi nchini Uganda wamemkamata kiongozi wa upinzani nchini humo Kizza Besigye na kumzuia kuingia mji mkuu Kampala.
Besigye alikuwa akienda kwa makao makuu ya chama hicho cha FDC katika eneo la Najjanankumbi kwa maombi, lakini polisi walikamata gari lake na kumzuia kwenda.
Gari ya Bw Besigye limebururwa na gari la polisi na kuelekezwa kituo cha polisi cha barabara ya Kira.
Hii si mara ya kwanza kuzuiliwa kwa kiongozi huyo ambaye amekuwa amekuwa akizuiliwa nyumbani kwake Kisangati, viungani mwa mji wa Kampala, tangu kufanyika kwa uchaguzi mkuu nchini humo Februari.
0 comments:
Chapisha Maoni