SAKATA la kutupwa lumande diwani wa kata ya Lusungo,Veronika Kanyanyila (CCM) kilichofanywa na mkuu wa wilaya ya Kyela Mbeya,Dr,Thea Ntara,limechukua sura mpya baada ya chama cha mapinduzi (CCM) kuketi na kulaani kitendo hicho.
Chama cha mapinduzi kupitia katibu wake wa siasa itikadi na uenezi,Richard Kilumbo,walifanya kikao na kulaani kitendo hicho na kudai kuwa mikakati ya kudhibiti ugonjwa huo unaofanywa na mkuu wa wilaya chama hakijapata walaka wowote.
Kilumbo alisema anakanusha kitendo cha mkuu huyo wa wilaya kwenda redioni akimtaja Mbunge wa jimbo hilo,Dr,Harrison Mwakyembe na mwenyekiti wa halmashauri kuwa wanaunga mkono kitendo cha yeye kumtupa lumande diwani huyo.
Hata hivyo chama kimatoa agizo la kutoruhusu mgogoro huo kuongelewa redioni wakisubiri mkuu wa mkoa afike na kutafuta ufumbuzi juu ya suala hilo,
Katibu huyo wa siasa na uenezi,licha ya kukiri kuwepo na ugonjwa huo wa kipindupindu wilayani humo,alisema mkuu huyo wa wilaya alishindwa kuzuia mikusanyiko siku ya sikuu ya pasaka ambapo mikusanyiko na sherehe mbalimbali zilifanyika kwenye kumbi za starehe.
BAADA YA HABARI HIYO HAYA HAPA NI BAADHI YA MATAMKO YA CHAMA YALIYOTOLEWA
(1)MH DC hakutoa waraka kwa madiwani na watendaji kukataza baadhi ya shughuli za jamii zinazochangia kuenea kwa kipindupindu pia hakueleza wajibu wa watendaji na madiwani katika kupambana na kipindupindu
(2) chama kimejiridhisha kuwa DC alikurupuka na kumdhalilisha mh kanyanyila kwa maneno ya kuambiwa
(3) Mtendaji wa kata aliyetumia zoezi la kipindupindu kukusanya pesa tozo za faini bila kutoa risiti wala hakuziwakilisha halmashauri
(4) Mbunge/mwenyekiti wa ccm/halmashauri hajaunga mkono kitendo cha kumdhalilisha diwani
0 comments:
Chapisha Maoni