Alhamisi, Februari 04, 2016

KUTEMBEA KWA MGUU KUNAWEZA KUKUEPUSHA KA KISUKARI

Kituo cha utafiti wa saratani cha taifa cha Japani hivi karibuni kimesema, hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari inayowakabili watu wanaotembea kwa miguu kwa muda usiozidi dakika 30 kila siku ni mara 1.23 ya ile ya watu wanaotembea kwa saa mbili au zaidi kwa siku.
Kikundi cha utafiti cha kituo hicho kiliwachunguza watu walioshiriki kwenye utafiti wa ugonjwa wa kisukari kuanzia mwaka 1998 hadi mwaka 2000. Baada ya kuwaondoa wale wanaojitambua kupata ugonjwa wa kisukari, watafiti waliwachunguza watu elfu 26 wanaodhani hawajapata ugonjwa huo.
Umri wa wastani wa watu hao ni miaka 62, na asilimia 36 kati yao ni wanawake. Baada ya kupima, watu 1,058 kati yao walithibitishwa kuwa na ugonjwa wa kisukari, lakini hawafahamu.

0 comments:

Chapisha Maoni