Serikali ya China imejenga shule mbili za kisasa ndani ya vyuo vikuu vya Dar es Salaam na Dodoma nchini Tanzania.Ujenzi wa shule hizo za msingi uligharimu dola milioni 23.3 chini ya mkataba wa ujenzi wa shule za msingi kati ya serikali ya China na mataifa ya bara Afrika.Wanafunzi watakaojiunga na shule hizo, ambazo zina vifaa vya kisasa vya mafunzo, watapata fursa ya kufundishwa lugha ya kichina kuanzia darasa la kwanza hadi la saba.
0 comments:
Chapisha Maoni