Ijumaa, Februari 05, 2016

KUELEKEA SIKU YA VALENTINE: VITU 17 AMBAVYO MWANAUME ANAHITAJI TOKA KWA MWANAMKE

1. Msalimie kwa tabasamu anaporudi nyumbani au mnapokutana. Usimsalimie huku umekunja sura, au huku unamtiririkia orodha ya vitu vya kufanya au unamlaumu kwa mambo ambayo hajayafanya.
2. Mnunulie kitu cha kuvaa ambacho atakipenda au ambacho kinaendana na vitu unavyojua anapenda. Mfano mkanda, t-shirt, pafyumu, saa, n.k. Kitu ambacho kila wakati akivaa anakukumbuka.
3. Muombee kwa Mungu afya njema na mafanikio huku akiwepo pamoja na wewe wakati wa maombi. Hakuna mwanaume ambaye hatavutiwa na kitu kama hicho.
4. Msifie mbele ya watoto wenu au kama hamna watoto mbele ya marafiki au ndugu. Inamfanya ajiamini zaidi na aongeze bidii na umakini kwenye mambo anayofanya, hatataka kufanya ujinga ujinga.
5. Msaidie wakati anavaa nguo. Mfano anapofunga tie yake au kufunga vifungo au mkanda. Usimsaidie tu kufungua mkanda wakati mnataka kufanya mapenzi lakini pia hata wakati anavaa kwa mishe mishe nyingine. Hii inaonyesha upendo wenu ni zaidi ya sex.
6. Msifie maumbile yake, kumbuka ni wewe peke yako na mama yake mzazi ambao mnamfahamu undani wake. Mwanaume anapenda kusifiwa namna alivyoumbwa, inampa confidence.
7. Mtumie SMS za kushtukiza ambazo zinampa furaha na ari ya bidii, mfano "Mpenzi, naona fahari na amani sana kuwa wako", mwanaume anayekupenda anafurahi kusikia maneno kama hayo toka kwako.
8. Mnunulie kitabu, movie au kitu cha kumjenga kifikra na kimtazamo. Inamfanya agundue kwamba wewe unampenda si tu kama alivyo bali unajali hata maendeleo yake kifikra na kimtazamo kama mpenzi, mumeo na baba wa wanao.
9. Mtoe sometimes. Muulize muda gani yuko free, nenda naye out. Mitoko sio ya wanaume tu kupanga, sometimes na wewe mwanamke chukua jukumu, inakujengea heshima na mapenzi yanadumu.
10. Jifunze kitu gani anapenda kula na mpikie mara kwa mara. Kaa na kula naye. Kisaikolojia, wanaume huwa wanakuwa na ukaribu mkubwa na watu wanaokula nao.
11. Mpangie mambo yake. Wanawake wako vizuri katika kupanga mambo (organizing). Kuwa mwanamke ambaye jamaa atakiri kwamba "Sijui maisha yangu yangekuwa vipi bila ya wewe, kuwa na wewe kwenye maisha kumefanya kila kitu changu kikae sawa".
12. Usivae vizuri sana ukiwa unatoka home kwenda kwenye ishu zako halafu ukiwa naye unavaa ovyo ovyo.
13. Muombe msaada kufanya baadhi ya mambo mara kwa mara hata kama unaweza kufanya. Wanaume hupenda kujisikia kwamba uwepo wao unahitajika, kama shujaa fulani vile.
14. Wafahamu marafiki zake wa karibu, wachukulie kama walivyo, usianze kupambana nao na kujaribu kumtenganisha nao. Muonyeshe kwamba unatambua nafasi yako katika maisha yake. Ishi katika mwenendo mzuri kiasi kwamba hata marafiki zake utasikia wanamwambia, "Brother, una bahati sana kupata mwanamke kama huyu maishani".
15. Mwambie kwamba unamuamini. Unamuamini katika matendo na unaamini ndoto zake na bidii yake katika kutafuta maisha. Mnapokuwa na shida mwambie kwamba unaamini solution itapatikana. Usiwe wewe ndo wa kwanza kumdharau, kumfokea, kumzidishia stress.
16. Kuwa fundi kitandani, fahamu anachopenda na kuwa fundi katika hicho kwenye mapenzi.
17. Kuwa amani yake. Katika yote unayofanya, jiulize: "Hivi huyu mtu anajisikia ana amani kuwa na mimi?" Mambo ya kubamiza milango, kununa nuna bila sababu, kumuimbia mipasho ya masimango vinamnyima amani.

0 comments:

Chapisha Maoni