Serikali ya Tanzania imesema kuwa ifikapo Juni 16, mwaka huu itavifungia vifaa vya mawasiliano vya mkononi haswa simu na tableti ambavyo vinatumia namba za usajili bandia, mamlaka ya mawasiliano nchini Tanzania(TCRA)ilisema siku ya Jumatano.
Meneja wa mawasiliano makao makuu innocent mungy, aliiambia shirika la habari la xinhua kuwa serikali ya Tanzania tayari imezindua mfumo wa rajisi ya namba za utambulisho wa vifaa vya mawasiliano na inawataka watoa huduma wa mawasiliano yanayotumia vifaa vya mkononi kuweka mfumo wa kudumu wa kumbukumbu za namba tambulishi ya vifaa hivyo (IMEI)
Serikali imetetea hatua hiyo na kusema kuwa ni moja wapo ya njia ya kudhibiti wizi wa simu na kuhimiza utii wa sheria nchini.
0 comments:
Chapisha Maoni