Afrika Kusini inafikiria kujiondoa kwenye mkataba wa Roma unaounda mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa jinai- ICC kwa madai ya kuwa mahakama hiyo inakandamiza bara la Afrika, waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Nkoana-Mashabane alisema siku ya Alhamisi mjini Pretoria.
Waziri huyo alizidi kusema kuwa hatua hiyo ya kujiondoa kutoka kwa mahakama hiyo itakuwa ya ushauriano mkubwa na ya taratibu.
"Tutahakikisha kwamba tumeshauriana na mashirika muhimu na kufanya hitimisho mwishoni," Nkoana-Mashabane alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni