1. Iwapo gari lako litaharibika, au kupata pancha, jaribu na lisogeze gari lako nje ya barabara. Kama hili haliwezekani liweke gari karibu na ukingo wa kushoto wa barabara na mbali ya makutano, madaraja na kona na sehemu nyingine za hatari.
2. Iwapo huwezi kuepuka kusimama barabarani LAZIMA utoe tahadhari kwa magari mengine kwa kuweka kiashiria chekundu cha pembetatu karibu na ukingo wa barabara si chini ya umbali wa m30 nyuma ya gari - pamoja na kiashiria kingine cha pembe tatu katika umbali uleule mbele ya gari. Pia lazima utumie taa zako za tahadhari ya hatari (indiketa mbili - zote zikiwaka kwa pamoja). Iwapo umesimama kwenye kona au karibu ya kilele cha kilima mtu moja arudi nyuma barabarani kuyatahadharisha magari Yanayokuja.
3. LAZIMA ujaribu na kuliondoa gari haraka iwezekanavyo. Ofisa wa polisi ana mamlaka ya kupanga namna ya kuliondoa gari lolote iwapo ataona linahatarisha usalama. Utapaswa kulipa gharama za kuliondoa.
4. Jaribu kutosimama au kutoshughulika na gari mahali ambapo utakuwa katika hatari ya kugongwa na magari yanayopita.
Unapolitengeneza gari usimwage dizeli au mafuta mengine barabarani, kwani yanaweza kuiathiri barabara.
5. Fanya kila jitihada kulitengeneza gari au kuliondoa barabarani. Kabla ya giza kuingia. Iwapo utalazimika kuliacha gari bovu
barabarani usiku, washa taa za kuegeshea na hakikisha kuwa kuna vibao vya tahadhari vya pembetatu vilivyowekwa umbali unaofaa barabarani kabla ya gari kuwatahadharisha madereva wengine. Waarifu Polisi.
6. Hakikisha kuwa mawe uliyotumia kuzuia matairi ya gari yameondolewa barabarani wakati unapoondoka.
0 comments:
Chapisha Maoni