Jumamosi, Januari 16, 2016

BAADA YA KUENGULIWA UNAHODHA, CANNAVARO AIBWAGA STARS

Nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ na klabu ya Yanga Nadir Haroub ‘Cannavaro’ ameamua kustaafu kuichezea timu hiyo ili kuweka nguvu kwenye klabu yake Yanga
Cannavaro amesemal yapo mambo mengi yaliyomfanya ajiondoe kuichezea timu hiyo moja wapo ni kitendo kilichofanywa na kocha mkuu wa timu hiyo Charles Boniface Mkwassa kumteua mshambuliaji Mbwana Samatta kuwa nahodha bila kumpa taarifa kabla na kingine ni lawama anazopata kutoka kwa mashabiki ambao wanadai yeye ndiye anayeifungisha timu hiyo.

0 comments:

Chapisha Maoni