Jumanne, Januari 12, 2016

BAADA YA BANGO LA KIBAGUZI LEO KATIKA MAPINDUZI DAY, CCM YANENA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.
Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

0 comments:

Chapisha Maoni