Jumanne, Januari 12, 2016

WATAKA KARUME AFUTWE UANACHAMA CCM ZANZIBAR

UMOJA wa vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), umekitaka chama hicho kumvua uanachama Rais mstaafu wa Zanzibar Dk Amani Abeid Karume. Kauli hiyo imetolewa katika viwanja vya Maisara mjini Zanzibar na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa, Sadifa Juma Khamis wakati wa kilele cha matembezi ya vijana wa umoja huo kuadhimisha miaka 52 ya Mapinduzi. Alimshushia tuhuma nzito mstaafu huyo kuwa anashirikiana na wapinzani kukihujumu chama hicho kikongwe nchini, na kwamba asipofukuzwa umoja umoja huo utatumia njia zingine ambazo hakuziweka wazi. Sadifa alionya kwamba Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar si mali wala miliki ya mtu kwani Wazanzibar wote wana haki ya kushiriki kuyaenzi kwa vitendo kutokana na historia yake.
 

0 comments:

Chapisha Maoni