Wapenzi wa gari za kisasa waliohudhuria maonyesho ya kimataifa ya
magari jijini Detroit, Marekani walivutiwa na ubunifu wa teknolojia za
kisasa kwenye magari yaliyokuwa katika maonyesho hayo, ikiwemo magari
yaliyo na uwezo wa kujiendesha bila dereva.
Magari ya Ford na
Volvo yaliongoza katika ubunifu wa teknolojia huku kampuni hizo mbili
zikionyesha teknolojia ya juu zaidi ya kuzuia visa vya ajali na magari
yanayojiendesha.
Jeshi la Marekani pia lilileta lorry yake yenye
uwezo wa kujiendesha, lakini teknolojia hio bado haitatolewa kwa
matumizi ya umma.
0 comments:
Chapisha Maoni