Staa wa filamu za Kibongo, Muhsein Awadhi ‘Dk. Cheni’ amekanusha tabia
ya wasanii wakubwa kuwaomba rushwa ya ngono wasanii chipukizi na kudai
wanaziendekeza wao wenyewe.
Akipiga stori na paparazi wetu, Dk. Cheni alisema yeye hajawahi
kumuomba msanii rushwa ya ngono, isipokuwa anaamini walio wengi
huanzisha mahusiano yaliyo rasmi kwa makubaliano yao kutokana na hisia
zinavyowasukuma.
Sidhani kama ni rushwa ya ngono, naamini wengi wanakubaliana, sehemu ya watu wengi mnapokutana inatokea watu kupendana na kuwa wapenzi hilo nakubali sababu ni jambo la kawaida hata wasanii kwa wasanii kupendana, sidhani kama mtu anaweza kulazimishwa kufanya mapenzi ili acheze filamu, mpaka watu kufanya tendo hilo wameshakubaliana
alisema Dk. Cheni.
0 comments:
Chapisha Maoni