Jumapili, Oktoba 19, 2014

TANZANIA INAKABILIWA NA UHABA WA MATABIBU WA MAGONJWA YA AKILI

RAIS wa Chama cha Wauguzi Tanzania, Paul Magesa amesema lipo tatizo la uhaba wa wauguzi nchini hasa wanaoshughulikia wagonjwa wa akili. Akizungumza na Fichuo Tz ofisini kwake Dar es Salaam jana, Magesa alisema idadi ya wagonjwa wa akili inaongezeka wakati hakuna wauguzi wa kutosha kwa ajili yao.
Kwa mujibu wa rais huyo, sensa iliyofanyika mwaka 2012 katika hospitali ya Mirembe mkoani Dodoma, ilionesha kwamba wauguzi wa wodi za wagonjwa wa akili wapo 502 wanaowahudumia wagonjwa zaidi ya 700.

Kumhudumia mgonjwa wa akili ni kazi ngumu mno lazima muuguzi apate elimu ya eneo hilo kwanza lakini hapa Tanzania hakuna shule wala chuo cha uuguzi kinachotoa elimu maalum kumuandaa muuguzi kwenda kumhudumia mgonjwa wa akili.
Mfumo wa maisha ulipo sasa watu wengi wanaangukia kwenye maradhi ya akili kutokana na msongo wa mawazo hivyo lazima muuguzi afahamu kuhusu matatizo hayo kabla ya kutoa huduma kwa mgonjwa.
…Wapo wauguzi waliomwagiwa vinyesi na wagonjwa, wanapigwa wakati mwingine mgonjwa anamtukana muuguzi sasa huyo mtoa huduma asipopewa elimu na akawa mvumilivu hataweza kutoa huduma wala kumshitaki sababu ni mgonjwa wa akili
alisema Magesa na kuongeza inahitaji moyo na motisha kuwahudumia wagonjwa wa aina hii.
Rais wa chama hicho alitumia muda huo kuiomba serikali iwe na mtaalam maalum kwa ajili ya wauguzi wataokwenda kuwahudumia wagonjwa wa akili badala ya hali ilivyo sasa ambapo muuguzi anapewa dondoo kisha anapelekwa kazini.

0 comments:

Chapisha Maoni