Jumatatu, Oktoba 20, 2014

MATUKIO MATATU MAKUBWA KUTOKA MBEYA LEO

KATIKA TUKIO LA KWANZA:

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha iduda wilaya ya mbozi aliyefahamika kwa jina la maneno wenela (35) aliuawa kwa kukatwa na kitu chenye makali sehemu za kichwani na shingoni na mtu/watu ambao majina yao yanahifadhiwa kwa sababu za kiupelelezi.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 19.10.2014 majira ya saa 13:15 mchana huko katika kijiji cha idunda, kata na tarafa ya iyula, wilaya ya mbozi, mkoa wa mbeya. Inadaiwa kuwa, chanzo cha mauaji hayo ni kulipiza kisasi.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi kwani ni kinyume cha sheria.

KATIKA TUKIO LA PILI:

Mtu mmoja mkazi wa kijiji cha katunduru wilaya ya rungwe aliyefahamika kwa jina la anna msyani (67) amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na gari lenye namba za usajili t.740 bzm aina ya toyota coaster likiendeshwa na dereva aitwaye vosta mwampegete (31) mkazi wa nzovwe.
Ajali hiyo imetokea mnamo tarehe 19.10.2014 majira ya saa 17:30 jioni huko katika kijiji cha lugombo, kata ya ilimi, tarafa ya pakati, wilaya ya rungwe, mkoa wa mbeya katika barabara ya tukuyu/kyela.
Inadaiwa kuwa, chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi. Dereva amekamatwa na gari lipo kituoni. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya wilaya ya rungwe.
Kamanda wa polisi mkoa wa mbeya kamishina msaidizi mwandamizi wa polisi ahmed z. Msangi anatoa wito kwa madereva kuwa makini wanapotumia vyombo vya moto ikiwa ni pamoja na kuzingatia sheria na alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoweza kuepukika. Aidha, anatoa wito kwa watembea kwa miguu na watumiaji wengine wa barabara kuzingatia alama za usalama barabarani ili kuepuka ajali zinazoepukika.

KATIKA TUKIO LA TATU:

Maduka matatu yaliyopo katika jengo moja liitwalo “kibona” yameteketea kwa moto na kusababisha uhabifu mkubwa wa mali zilizokuwemo katika maduka hayo na hasara kwa wamiliki wake.
Tukio hilo limetokea mnamo tarehe 19.10.2014 majira ya saa 23:00 usiku huko maeneo ya kyela kati, kata ya kyela, tarafa ya unyakyusa, wilaya ya kyela, mkoa wa mbeya.
Maduka yaliyoteketea kutokana na moto huo ni pamoja na duka la vifaa vya ujenzi, duka la pembejeo pamoja na stationery. Aidha, wakati wa ajali hiyo wamiliki wa maduka hayo hawakuwepo katika eneo la tukio.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana. Aidha, thamani halisi ya mali iliyoteketea kwa moto bado kufahamika. Hakuna madhara ya kibinadamu yaliyoripotiwa kutokea. Moto huo ilizimwa kwa ushirikiano wa askari polisi na wananchi.

0 comments:

Chapisha Maoni