Kiwango cha walimu wanaokwenda kinyume na maadili na kufutwa kazi kimeendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka, ambapo katika kipindi cha mwaka 2013/2014 walimu 422 wamefutwa katika maeneo mbalimbali nchini, wakiwemo watatu kwa kubainika kujihusisha kimapenzi na wanafunzi na wawili kwa kuwaonesha wanafunzi mitihan, ikilinganishwa na walimu 278 mwaka 2012/2013.
Katibu msaidizi wa idara ya utumishi wa walimu, Christina Hape, amesema hayo mjini Morogoro, na kubainisha kuwa mwaka 2012/2013 walifutwa kazi asilimia 98 ya walimu 151 ambao mashauri yao yalipelekwa katika idara hiyo kwa mapendekezo ya kufutwa kazi, ambapo amesema sababu kubwa ya walimu kufutwa kazi ni utoro unaotokana na wengi kwenda kujiendeleza kielimu bila ruhusa ya mwajiri.
Amesema makosa makubwa yakiwemo ya mwalimu kubainika kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanafunzi ama kuonesha mitihani, husababisha mwalimu kufukuzwa kazi sambamba na utumishi serikalini na binafsi, huku makosa mengine kama utoro, mwalimu akifukuzwa kazi na kuachiwa utumishi wake.
Naye kaimu katibu mkuu wa tume ya utumishi wa umma, ambaye pia ni naibu katibu idara ya utumishi, Rose Elipenda, ametoa wito kwa waajiri kusimamia vyema utumishi wa watumishi, kwa kuzingatia sheria, taratibu na kanuni za kazi na kushughulikia changamoto zinazojitokeza katika maeneo yao ya kazi kabla ya kufikisha mashauri yao katika mamlaka za juu kwa maamuzi zaidi.
Kwa mujibu wa taarifa ya idara ya utumishi wa walimu, watumishi hao wanapaswa kuhakikisha wanatii mamlaka za kisheria zilizowaweka katika nafasi zao sambamba na kuzingatia kuwa ualimu sio taaluma pekee bali pia suala zima la maadili kwani wakimpotosha mtoto wanayeaminiwa kumjenga kiakili, ni kupotosha taifa zima.

0 comments:
Chapisha Maoni