Jumapili, Oktoba 19, 2014

SUGU AMCHARUKIA SITTA KWA KUMSALITI

Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA), Joseph Mbilinyi ameeleza ulaghai alioutumia Samuel Sitta kupata ushindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba na kumfanya Andrew Chenge kujiondoa kwenye kinyang’anyiro hicho.
Akihutubia mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Miono mkoani Pwani juzi, Mbilinyi maarufu kama Sugu alisema Sitta katika kampeni zake alikwenda kwa wajumbe usiku na mchana akitumia mbuni mbali mbali za kujinadi kuwa angetenda haki kwa pande zote.

Mimi nilifuatwa na Sitta saa saba usiku mjini Dodoma nikiwa na mbunge wa Arumeru Mashariki, Joshua Nassari, akanitaka nimsaidie kuwashawishi wajumbe vijana hususan wa upinzani, akidai Chenge ni muuminiwa serikali mbili kama msimamo wa chama chake ulivyo.
Sitta ni mnafiki sana, alitafuta kura kwa kurubuni wajumbe hasa wa upinzani akidai yeye muumini wa serikali tatu; mnaona ulaghai huo ndugu zangu
alisema.
Sugu aliongeza kwamba, baada ya ushawishi huo, alikubaliana naye huku akimewondolea mashaka kuwa angeweza kuwasaliti wakati wa kuendesha Bunge hilo.
Nilimuuliza kabla sijakubaliana naye, mzee unasema kweli kwamba hutatusaliti, akasema ndio… mimi nimekuwa mtetezi wa wanyonge siku zote, huyo Chenge hawezi kusimama kwa wote, nisaidie…nikabali na kweli tulimchagua lakini cha kushangaza baada tu ya kukalia kiti akabadilika
asema.
Kuhusu uchakachuaji wa rasimu ya Jaji Joseph Warioba ambayo ndiyo ilikuwa na maoni ya wananchi, Sugu alisema ulianzia kwa Sitta kutumia ulaghai kwa wajumbe wa bunge hilo akifanya kampeni achaguliwe kwa faida ya chama chake.
Rais Jakaya Kikwete namhurumia sana, hii ndiyo ilikuwa kete yake kwa Watanzania ya kujivunia katika utawala wake, maana marais wote waliopita wanayo mambo ya kujivunia yanayowafanya waendelee kukumbukwa, kwa Rais Kikwete ilikuwa ni hii…sasa ameivuruga
alisisitiza.
Awali, aliyekuwa mgombea wa ubunge wa Chalinze katika uchaguzi mdogo wa mwaka huu, Mathayo Torongey (CHADEMA), aliwataka wananchi wa jimbo hilo kuacha kulalamika na badala yake wachukue hatua katika uchaguzi ujao.
Alisema kuwa wananchi wamekuwa wakimlalamikia mbunge wa sasa Ridhiwani Kikwete kuwa hajatimiza ahadi zake ikiwemo kununua trekta kila kijiji na kwamba tangu achaguliwe ameshindwa kutoa kushukurani kwa wananchi waliompa kura.

0 comments:

Chapisha Maoni