Alhamisi, Oktoba 30, 2014

JESHI LA POLISI MKOA WA MBEYA LAENDELEA KUKAMATA POMBE KALI

Jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linawashikilia watu wanne waliofahamika kwa majina ya 1. Othaz Angolile (18) 2. Samson Mwangomile (46) 3. Ford Samson (20) na 4. Baraka Joseph (23) wote wakazi wa Airport jijini Mbeya wakiwa na pombe kali zilizopigwa marufuku nchini aina ya Boss na Ridder paketi 108.
Watuhumiwa walikamatwa katika msako uliofanyika jana majira ya saa 11:00 asubuhi katika mtaa wa Airport, kata ya Iyela, tarafa ya Iyunga, jiji na mkoa wa Mbeya. Watuhumiwa ni wauzaji wa pombe hizo na taratibu za kuwafikisha mahakamani zinaendelea.
Kamanda wa polisi mkoa wa Mbeya Ahmed Msangi anatoa wito kwa jamii kuacha kutumia/kuuza pombe kali zilizopigwa marufuku na serikali kwani ni kinyume cha sheria na ni hatari kwa afya ya mtumiaji.

0 comments:

Chapisha Maoni