Mwanamke mmoja mwenye watoto watatu
katika wilaya ya kole nchini Uganda alimuandalia mumewe mlo wa mipira ya
kondomu kufuatia ugomvi usiokwisha.
Mwanamke huyo ambaye ni
mkaazi wa eneo la Arao aliripotiwa kununua paketi tatu za kondomu aina
ya Trust kutoka duka jirani kabla ya kuzipika na kumuandalia mumewe kama
chakula baada ya kurudi nyumbani akiwa amelewa chakari.
kulingana
na gazeti la bdaily monitor nchini Uganda inadaiwa kuwa mwanamke huyo
aliikata kata mipira hiyo ya kondomu ambayo ilikuwa haijatumika katika
vipande vidogo vidogo na kuvichemsha kwa mda kabla ya kuvikaranga na
mafuta ya kupikia na viungo vyenginevyo.
Wakati mumewe alipowasili
kutoka kubugia pombe katika eneo jirani la kibiashara la
Odede,aliandaliwa mlo huo katika sahani tofauti moja ikiwa na mipira
hiyo kama mboga na nyengine ikiwa na makaa.
Lakini jamaa huyo alibaini njama za mkewe baada ya kuonja mlo huo na kugundua ulikuwa na ladha tofauti.
Hatua hiyo ilikuwa ikilenga kumfunza mume huyo ambaye amedaiwa kuzua ugomvi na mkewe kila anapolewa na kurudi nyumbani.
0 comments:
Chapisha Maoni