Gari moshi(treni) limeacha njia yake na kuanguka kuhu likiwa limebeba mabehewa Vingunguti jijini Dar es Salaam.
Taarifa zina bainisha kuwa njia hiyo ya Treni ni mbaya kwa
kuchimbika chimbika nahivyo kusababisha mkwamo kwenye treni hiyo na
hivyo kulazimika kuanguka huku tairi zake kuchomoka na kila moja kuwa
upande wake.
Katika msemo wa kufa kufaana panapo tokea ajali,iliweza kuwalazimu
askari wa kutuliza ghasia kufika mara moja eneo hilo la vingunguti kwa
lengo lakuweka ulinzi dhidi ya wanaoweza kutia hasara kwa kuondoka na
bhaadhi ya vyuma kwenye treni hiyo.
Mashuhuda wa walioshuhudia ajali wanasema kuwa njia ya treni hiyo
si salama sana,na hivyo njia kupelekea hadi kuanguka na wataalamu
wanasema Pin Lock ndio iliyo sababisha pia kuweza kushindwa treni kukaa
kwenye njia yake baada ya kukatika. Haijafahamika Mabehewa yalikuwa na nini ndani yake.
0 comments:
Chapisha Maoni