Maiti ya mtu ambaye hajatambulika imeokotwa ikiwa na majeraha makubwa katika maeneo ya usoni ikisadikiwa kuwa ameuawa na watu wasiofahamika kwa kukatwa na kitu chenye ncha kali katika cha Ilolo wilaya ya Mbozimkoani Mbeya.
Kwa mujibu wa jeshi la polisi mkoani Mbeya, tukio hio limetokea jana asubuhi majira ya saa moja na nusu huku ikidaiwa kuwa chanzo cha tukio hilo ni tuhuma za wizi lakini pia katika eneo hilo la tukio pamekutwa na godoro moja jipya, mashukamawili pamoja na sketi nyeusi.
Baada ya jeshi la polisi kufika katika eneo la tukio askari waliuchukua mwili wa marehemu na kuuhifadhi katika hospitali ya serikali ya Vwawa kwa uchunguzi zaidi pamoja na kutambuliwa na ndugu kwaajili ya shughuli za mazishi.
Kamanda wa polisi mkoani Mbeya, Ahmed Msangi ameithibitishia Fichuo Tz juu ya tukio hilo na kutoa wito kwa yeyote mwenye taarifa za watu waiohusika katika tukio hilo azitoe katika mamlaka husika ili wakamatwe na sheria ichukue mkondo wake.
0 comments:
Chapisha Maoni