MSIKITI wa Mtambani uliopo Kinondoni jijini Dar es Salaam, umeteketea
tena kwa moto, huku bweni la wanafunzi wa kike pia likiathirika na moto
huo ambao hata hivyo haukusababisha madhara yoyote kwa binadamu.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni, Camellius Wambura
amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amedai kuwa chanzo cha moto huo
bado haujafahamika.
Akizungumza katika eneo la tukio, Camellius Wambura alisema moto huo ulitokea majira ya saa 6 mchana na ulianzia kwenye chumba kimoja kinachotumiwa na wanafunzi wa kike wa kidato cha nne kwa ajili ya kujisomea.
Aliongeza kuwa chumba hicho hakikuwa na mtu wakati tukio hilo
linatokea, huku akiweka wazi kuwa moto huo umeteketeza magodoro manne
ambayo yalikuwa yakitumiwa na wanafunzi hao wa kike.
Alidai kuwa
chanzo cha moto huo bado hakijafahamika, huku jeshi la polisi
linaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini chanzo cha moto huo.
0 comments:
Chapisha Maoni