Jumamosi, Agosti 30, 2014

WILAYA YA IRINGA YATUMIA BIL.7.2 KUBORESHA MIUNDOMBINU

Halmashauri ya wilaya ya Iringa Mkoa wa Iringa imetumia zaidi ya shilingi ya bilioni 7.2 kwenye uboreshaji na ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo kati ya mwezi Januari hadi Juni mwaka 2014.
Mkuu wa wilaya ya Iringa Dkt. Leticia Warioba amesema kwenye kikao cha tathimini kuwa katika kipindi hicho miradi ya afya na elimu imetumika zaidi ya shilingi milioni 200 ambayo ni kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara za Maeneo ya Wenda hadi Mgama yenye urefu wa kilomita 19.7.
Dkt. Warioba ameongeza kuwa kwa upande wa sekta ya afya halmashauri ya wilaya ya Iringa imefanikiwa kusambaza dawa na vifaa mbalimbali vya tiba kwenye vituo 66 vya afya na hospitari za serikali ili viondokane uhaba huo.
Aidha, amesema, kwa upande wa elimu wilaya ya Iringa pia imetoa zaidi ya vitabu 254 ambavyo ni vya kiada na ziada kwenye shule za msingi 145 ili kuongeza ufaulu wa wanafunzi kwa shule hizo.
Hata hivyo, mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilaya ya Iringa Vijijini Mkoa wa Iringa Bibi Delfina Mtavilalo amewakumbusha viongozi wa idara mbalimbali Mkoani Iringa kuwa na umoja katika kuwaletea wananchi maendeleo.

0 comments:

Chapisha Maoni