Jumamosi, Agosti 30, 2014

KATA YAAMUA KUJIJENGEA SHULE YA MSINGI YA KIINGEREZA IRINGA

Uongozi wa kata ya Gangilonga Manispaa ya Iringa umependekeza kujengwa kwa shule ya msingi ambayo ni mbadala kwa mchepuo wa lugha ya kiingereza ya Shule ya Msingi Mapinduzi katika kata hiyo kutokana na wingi wa wanafunzi.
Diwani wa Kata ya Gangilonga Manispaa ya Iringa Bi Nicolina Lulandala amesema, licha ya shule hiyo kuwa na idadi kubwa ya wanafunzi kwa kipindi kifefu imekuwa ikifanya vizuri kwenye matokeo ya mitihani ya kitaifa.
Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Mhe. Mchg. Peter Msigwa amesema kuwa ataendelea kushirikiana na viongozi wa kata hiyo ili kutatua tatizo lao.
Kaimu Mkurugenzi manispaa ya Iringa amesema, hatua hiyo itasaidia kuleta ufanisi kwa wanafunzi kwenye masomo yao hasa ya sayansi aidha ametoa wito kwa wadau wengine wasaidie kuchangia sekta ya elimu ili kukuza kiwango cha sekta hiyo.
Hata hivyo, Diwani Lulandala amemuomba mbunge wa Iringa Mjini kuendelea kuhamasisha serikali ili waweze kuwekeza zaidi kwenye suala la utalii kwani kata hiyo ina vivutio vinavyoweza kuingiza kipato zaidi.

0 comments:

Chapisha Maoni