BARAZA la Mitihani la Taifa (NECTA), limetangaza mfumo mpya wa
upangaji wa madaraja ya ufaulu kwa kutumia wastani wa pointi (GPA) ambao
utaanza kutumika katika mtihani wa kidato cha nne 2014 na cha sita
2015.
Akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari jana jijini Dar es
Salaam, Katibu Mtendaji wa NECTA, Dk. Charles Msonde, alisema kuwa mfumo
huo umekuwa ukitumika katika kupanga madaraja ya ufaulu katika baadhi
ya mitihani inayosimamiwa na baraza hilo.
Alisema manufaa yake ni kuwa na mfumo wa kutunuku matokeo wa ina moja
katika ngazi zote za mafunzo kuanzia elimu ya msingi hadi elimu ya juu;
matokeo yaliyo katika mfumo huo kwenye cheti yatarahisisha kazi ya
udahili wa watahiniwa unaofanywa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU) na NACTE
katika ngazi za juu za mafunzo.
Pia aliongeza kuwa mfumo wa GPA ni rahisi kuelewa kwa wadau wa kada
mbalimbali kwa sababu hutoa tafsiri yenye kuonesha mtahiniwa aliye na
GPA kubwa ndiye aliye na maokeo mazuri.
Kwa mujibu wa Dk. Msonde, madaraja katika mfumo wa GPA hupangwa
katika utaratibu wa Distinction, Merit, Credit na Pass ambapo daraja la
juu ufaulu ni Distinction na la chini ni Pass.
Kulingana na utaraibu huo, daraja la Distinction litakuwa na alama
kati ya 3.6-5.0, Merit 2.6.3.5,Credit 1.6-2.5, Pass 0.3-1.5 na Fail
0.0-0.2 kwa matokeo ya kidato cha nne wakati wa kidato cha sita
Distinction ni kati ya 3.7-5.0, Merit 3.0-3.6, Credit 1.7-2.9, Pass
0.7-1.6 na Fail 0.0-0.6.
“Ukokotoaji wa wastani wa pointi (GPA) ya mtahiniwa hufanywa kwa
kuzingatia masomo ambayo mtahiniwa amefaulu. GPA anayopata mtahiniwa wa
mtihani wa kidato cha nne hutokana na wastani wa pointi alizopata katika
masomo saba aliyofaulu vizuri wakati kwa kidato cha sita ni masomo
matatu,”alisema.
0 comments:
Chapisha Maoni