Chelsea wameanza mazungumzo na mshambuliaji wa
QPR Loic Remy, 27, baada ya Fernando Torres, 30, kwenda AC Milan
(Telegraph), kiungo wa Manchester United Tom Cleverly, 25, anafikiria
kwenda Aston Villa kwa pauni milioni 7, baada ya kuzungumza na nahodha
wa zamani wa Man Utd Roy Keane ambaye sasa ni meneja msaidizi Villa Park
(Daily Mirror), meneja mpya wa Crystal Palace Neil Warnock anataka
kumchukua beki wa QPR Armand Traore, 24, kwa pauni milioni 2.5 (Sun),
Arsenal wamepata matumaini makubwa ya kumchukua winga Alessio Cerci,
27, baada ya rais wa Torino, Urbano Cairo kusema mchezaji huyo atauzwa
kwa bei stahiki (Daily Star), Manchester United wanataka kumsajili beki
Timothy Fosu Mensah, 16, kutoka Ajax (Daily Express), uhamisho wa beki
Marcos Rojo, 24, kwenda Manchester United uko hatarini kutokana na
kutopata bado kibali cha kufanya kazi na pia wakala wa tatu wa uhamisho
aliyepo kwenye mkataba wake (Sun), West Ham wanakaribia kukamilisha
uhamisho wa Alex Song, 26, kutoka Barcelona kwa mkopo (Daily Mail),
Birmingham City wanataka kumchukua Hatem Ben Arfa, 27, kutoka Newcastle
kwa mkopo (Newcastle Chronicle), Manchester United wanahitaji kutoa
pauni milioni 5 zaidi kuweza kumsajili Arturo Vidal kutoka Juventus huku
klabu hizo mbili zikiendelea na mazungumzo kabla ya dirisha la usajili
kufungwa Jumatatu (Tuttosport), Benfica wanajiandaa kutoa pauni milioni
7.9 kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Joel Campbell (O Jogo), Manchester
United wamekubali kutoa pauni milioni 14.2 na Ajax kumchukua Daley Blind
(De Telegraaf), Chelsea wako tayari kuongeza juhudi kumfuatilia
mshambuliaji wa Roma Mattia Destro kufuatia kuondoka kwa Fernando Torres
(Daily Mirror). Zimesalia siku mbili kabla ya dirisha la usajili
kufungwa Jumatatu. Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa.
0 comments:
Chapisha Maoni