Mshindi wa mashindano ya taji la Miss Asia Pacific
World, May Myat Noe, amevuliwa taji lake akisemekana ni mjeuri, hana
hadhi na hastaili taji hilo.
May Myat Nwoe alivishwa taji lake mwezi Mei
baada ya kufanyiwa upasuaji na kuwekwa matiti bandia kufuatia ombi la
waandalizi wa mashindano hayo wa Korea.
Baadaye walimlaumu wakisema hataki kushirikiana nao na sasa wanataka aombe radhi na pia arejeshe taji alilovishwa.
Waandalizi walisema hawajafurahishwa na kitendo cha msichana huyo kumpeleka mamake nchini Korea Kusini.
May Myat Noe, mshindi wa kwanza wa tuzo hiyo kutoka Burma, sasa anaripotiwa kutoweka na taji alilovikwa aliposhinda mwaka jana.
Msemaji wa waliodhamini taji hilo anasema
msichana huyo wa miaka 18 alitoweka baada ya kufahamishwa uamuzi huo wa
kumpokonya taji hilo wiki jana.
BBC imefahamishwa kwamba waandalizi wa shindano hilo pamoja na mamake msichana huyo walitofautiana kuhusu usimamizi wake.
Shirika lilioandaa shindano hilo, limesema kuwa Bi May alidanganya na kwamba hana heshima kwa waandalizi wa shindano hilo.
Lilisema kukosa heshima kwake ni moja ya sababu za kumpokonya taji lake.
Kadhalika shirika hilo lilisema kuwa msichana
huyo, aliyekuwa amepata mikataba ya kufanya rekodi ya miziki pamoja na
kuigiza, alitoroka na taji lake lenmye thamani ya dola 100,000.
Mwandishi wa BBC Jonah Fisher anasema kuwa
mamake May alionekana kutaka kumsimamia msichana wake lakini chini ya
masharti ya shindano hilo, mshindi anapaswa kusimamiwa na waandalizi.
Inadhaniwa Bi May amerejea nchini Burma.
0 comments:
Chapisha Maoni