MBUNGE wa Kigoma Kaskazini, Kabwe Zitto (Chadema) amesisitiza
hajawahi kuwa katika kundi la Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wala
kundi lolote ndani ya Bunge Maalumu la Katiba isipokuwa, yuko kwenye
linalotaka maridhiano.
Hata hivyo katika taarifa yake kwa vyombo vya habari aliyoitoa jana,
Zitto alisema msimamo wake kuhusu mchakato wa kuandika Katiba mpya ni
kutohudhuria Mkutano wa Bunge Maalumu unaotarajiwa kuanza wiki ijayo,
kama makundi hasimu hayatafikia maridhiano.
Alisisitiza msimamo wake kuhusu Muungano kuwa ni serikali tatu
zilizoboreshwa kuwa na Muungano imara usio tegemezi wala egemezi kwa
washirika wake.
Mbunge huyo alikuwa akitoa kile alichosema ni ufafanuzi kuhusu
msimamo wake kulingana na mahojiano aliyofanyiwa katika kipindi cha
PowerBreakFast kinachorushwa na Clouds FM na hatimaye, mahojiano hayo
kuandikwa na baadhi ya vyombo vya habari.
Alisema Mkutano wa Bunge Maalumu utakaofanyika bila kuwepo kwa
maridhiano utakuwa hauna maana yoyote na itakuwa ni sawa na kupoteza
muda na fedha za walipa kodi ambazo zingeweza kununua dawa vijijini.
Hata hivyo, Zitto alisema anaunga mkono mgomo wa baadhi ya wajumbe wa
Bunge Maalumu la Katiba kupinga lugha za matusi na lugha za kibaguzi
zilizokuwa zinaendelea ndani ya mikutano.
Pia alisema anaunga mkono kwamba Rasimu inayopaswa kujadiliwa ni
iliyotokana na Tume ya Mabadiliko ya Katiba iliyoongozwa na Jaji Joseph
Warioba.
Zitto alisema kwa hali ya sasa kuna mkwamo katika kupatikana kwa
Katiba bora, unaotokana na kutokuwepo kwa nia ya dhati ya kupata
maridhiano ya pande zinazopingana.
Ukawa hawataki mazungumzo na viongozi wa Bunge la Katiba badala ya kujenga maridhiano kila siku wanawabeza Ukawa, jambo ambalo kamwe haliwezi kujenga mwafaka.Ushauri wangu ni kuahirisha mchakato mzima wa kuandika Katiba mpaka mwaka 2016 baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. Katiba ya sasa ifanyiwe marekebisho machache
alisema katika taarifa
yake.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge
ya Hesabu za Serikali (PAC), aliyataja marekebisho yanayotakiwa
kufanywa kwenye Katiba ya sasa kuwa ni pamoja na Tume ya Uchaguzi kuwa
huru kwa kuwaondoa watumishi wa Halmashauri za Wilaya, Miji na Majiji
katika kusimamia uchaguzi.
Marekebisho mengine ni,kuruhusu mgombea binafsi na kuondoa mafuta na
gesi kama jambo la Muungano ili Zanzibar ianze mara moja kusimamia kwa
uhuru utafutaji wa mafuta katika vitalu vilivyopo upande huo wa
Muungano.
0 comments:
Chapisha Maoni