Mabingwa wa Spain, Atletico Madrid wanataka kuwasajili Santi Cazorla,
29, kutoka Arsenal, Fernando Torres, 30, kutoka Chelsea na Chicharito,
26 kutoka Manchester United (Daily Star), Chicharito amekiri kuwa hana
uhakika kama ataendelea kuwepo Old Trafford akisema "Mungu pekee ndio
anajua" kuhusu hatma yake (Guardian), Tottenham wanatarajia kurejea na
fedha zaidi kumtaka kiungo wa Southampton Morgan Schneiderlin, licha ya
Saints kusema mchezaji huyo hatoruhusiwa
kuondoka (Daily Telegraph), Sporting Lisbon wamewaambia Southampton
kuwa watalazimika kutoa pauni milioni 16 kumsajili beki kutoka Argentina
Eric Dier, 20 (Daily Telepgraph), Marouanne Fellaini, 26 amekubali
kujiunga na Napoli ya Italia, lakini Manchester United wanataka pauni
milioni 18 kwa mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa pauni milioni 27.5 mwaka
jana (Daily Star), meneja wa Sunderland Gus Poyet amethibitisha kuwa
wameanza tena mazungumzo ya kumsajili Fabio Borini, 23, kutoka Liverpool
(Daily Express), Arsenal wanaweza kufufua mazungumzo ya kumsajili Sami
Khedira, 27, kwa kuwa Real Madrid wanataka kumuuza kiungo huyo (Daily
Mirror), Juventus wamekubali dau la pauni milioni 47 kutoka Manchester
United kumsajili Arturo Vidal, 27, na mchezaji huyo wa Chile amekubali
maslahi binafsi na Old Trafford (CaughtOffside), matumaini ya Newcastle
ya kumsajili mshambuliaji Alexandre Lacazette, 23, kwa pauni milioni 10
yamegonga mwamba baada ya mchezaji huyo wa Ufaransa kusaini mkataba mpya
na klabu yake (Newcastle Cronicle), Napoli wamewapa Manchester United
Dries Mertens kubadilishana na Marouanne Fellaini (Daily Express), Karim
Benzema amekubali kusaini mkataba mpya na Real Madrid hadi mwaka 2018
wenye thamani ya euro milioni 7 kwa mwaka (El Confidencial), Bayern
Munich wameanza kumfuatilia winga wa Real Madrid Angel Di Maria ambaye
anasakwa pia na Manchester United na Paris Saint-Germain (AS).
0 comments:
Chapisha Maoni