WATANZANIA wametakiwa kuwa makini
wanapotumia simu na kompyuta, kwani ndio chanzo cha matatizo mbalimbali
yakiwemo ya kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Mshauri wa masuala ya teknolojia, Alex
Mpompo aliyasema hayo juzi kwenye semina inayohusu teknolojia katika
Parokia ya Roho Mtakatifu Segerea, Jimbo Kuu la Dar es Salaam.
Mpompo alisema matatizo yanayochangiwa na teknolojia yapo mengi ikiwamo kutoona, kutosikia, upungufu wa nguvu za kiume na vifo.
Alisema vijana wengi nchini wana
upungufu wa nguvu za kiume jambo linalochangiwa na matumizi mabaya ya
teknolojia hivyo kuchangia familia kusambaratika.
Aliwaasa Watanzania kutotumia kompyuta
kwa muda mrefu kwa kuipakata kwenye mapaja, kwani mionzi inapenya kwa
urahisi katika maeneo hayo na kuathiri mbegu za kiume na kusababisha
ugumba.
Watu wengi hawaelewi kama ukiweka simu karibu na jiko la gesi unaweza kuunguza nyumba, pia unapogandamiza simu na ngozi inasababisha saratani ya matiti na ugonjwa wa moyo
alisema
Mpompo.
Alisema vijana wanaoongea na simu kwa muda mrefu wapo kwenye hatari zaidi ya kupoteza kumbukumbu na kutosikia.
0 comments:
Chapisha Maoni