Kwa kawaida mashabiki wa mpira wa miguu, mpira mikono, mpira wa
kikapu au hata ‘handball’ huingia kwa wingi uwanjani kushangilia mechi
kati ya timu zao na wapinzani. Lakini hii imekuwa tofauti kwa mashabiki
wa mpira wa Volleyball huko Taiwan.
Vyombo vya habari vya nchini humo vimeeleza kuwa wadau wa mpira wa
Volleyball wamemlalamikia mchezaji wa kike mrembo na mwenye mvuto haswaa
anaefahamika kwa jina la Sabina Altynbekova kuwa chanzo cha kuharibu
uhalisia na utamu wa mechi za mchezo huo pale timu yake inayoitwa
‘Kazakhstan’ inapokutana na timu nyingine.
Taarifa hizo zinaeleza kuwa umati wa mashabiki hasa wanaume
wanaonekana kuwa huingia uwanjani kumuangalia zaidi msichana huyo mwenye
umri wa miaka kati ya 17 na 18, na hivyo mvuto wake huharibu uhalisia
wa mechi kwa kuwa kila anaposhika mpira hushangiliwa sana kama ndiye
mchezaji pekee kitu ambacho kinaonekana kuwa tatizo hata kwa wachezaji
wenzake.
Kocha wa timu hiyo, Nurlan Sadikov pia ameonekana kusikitishwa na
hali hiyo inayoathiri saikolojia ya wachezaji wengine wa timu yake.
Haiwezekani ifanyike hivi…umati wa watu unafanya kama vile kuna mchezaji mmoja tu kwenye hii ligi hii ya mabingwa.
Kocha Sadikov
aliiambia Tengrin News.
Video ya sabina, Altynbekova iliwekwa YouTube wiki iliyopita na tayari imeshatazamwa zaidi ya 1, 153, 646.
0 comments:
Chapisha Maoni