Jumatano, Julai 30, 2014

BAADA YA LOWASA KUPEWA KASHFA NA 'TANZANIA DAIMA' ATOA TAMKO

Katika gazeti la Tanzania Daima toleo Na. 3536 la tarehe 30 Julai, kuna habari inayosema Lowassa aibukia ACT na kumuhusisha na Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Zitto Kabwe katika kile gazeti hilo kilichodai mikakati ya siri dhidi ya Chadema.
Habari hizo ni uzushi, na ni muendelezo wa mikakati ya kumchafua na kumgonganisha Mh Lowassa na wanasiasa wenzake wa kada na maeneo mbalimbali.
Mh Lowassa kama walivyo wabunge wengine wa CCM amekuwa na uhusiano na wabunge wenzake bila kujali tofauti ya vyama vyao.
Mh Lowassa ni kiongozi makini ambaye hawezi kupoteza muda wake kujiingiza katika masuala yasiyo na tija kwa nchi, wananchi na ustawi wa demokrasia makini na endelevu nchini.
Muda wake anautumia kusimamia utekelezwaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM jimboni kwake Monduli.
Mimi na chama chetu, tuko busy kutekeleza ilani yetu, kuwaletea maendeleo wananchi ili wazidi kutupa ridhaa ya kuwaongoza katika chaguzi zijazo
alisema Mh Lowassa.
Hata hivyo, Mh Lowassa anathamini mchango wa vyama vyote vya siasa nchini pamoja na Chadema katika kujenga demokrasia yenye tija kwa taifa.
Imetolewa na ofisi ya Mh Edward Ngoyi Lowassa (MB)

0 comments:

Chapisha Maoni