Mwimbaji wa Loyal, Chris Brown ambaye alitoka jela hivi
karibuni na kuamua kutafuta amani kwa kuhama nyumba aliyokuwa akiishi
kukwepa ugomvi na majirani zake ni kama ameruka majivu na kukanyaga
moto.
Kwa mujibu wa TMZ, mwimbaji huyo aliamua kuuza nyumba yake ya
kifahari iliyokuwa Hollywood Hills kufuatia ugomvi wa kila siku na
majirani zake waliomfikisha kwenye vyombo vya sheria mara kadhaa kwa
madai ya kuwanyima raha na familia zao kwa vitendo vyake. Baada ya kuuza
nyumba hiyo alinunua nyumba mpya, California.
Kwa bahati mbaya majirani wapya wa mwimbaji huyo wanaonekana kuwa na
maamuzi magumu zaidi ya wale wa awali waliokuwa wanampeleka kwenye
vyombo vya sheria.
Akiongea na TMZ, jirani mmoja alieleza kutofurahishwa kwake na ujio
wa Chris Brown kwenye ujirani wao na kuahidi kuwa endapo atagusa
nyumbani kwake atampiga risasi.
It can be the devil. I can care less.. I don’t care if they are having orgies. It can even be Sadam Hussein for all I care, as long as he doesn’t trespass onto my property. If he does, I shoot him.
Jumba jipya la Chris Brown lina vitu vya kifahari kama uwanja wa
kuchezea tennis, dance studio, club house, commercial ice cream bar na
mengine mengi huku eneo zima likuwa na ukubwa wa eneo la mraba futi
8,000 na vyumba sita vya kulala.
0 comments:
Chapisha Maoni