Jumatano, Julai 30, 2014

TAREHE YA LEO KATIKA HISTORIA

Miaka 34 iliyopita katika siku kama ya leo, nchi ya Vanuatu iliyoko mashariki mwa Australia ilipata uhuru. Mwanzoni mwa karne ya 17 visiwa vya Vanuatu vilidhibitiwa na Wahispania na mwishoni mwa karne ya 18 Waingereza na Wafaransa wakawasili katika visiwa hivyo. Kuanzia mwaka 1887 kulizuka mapigano baina ya wahajiri wa Kiingereza na Kifaransa waliokuwa wakiishi Vanuatu. Mwaka 1906, London na Paris zilikubaliana kuiendesha pamoja nchi hiyo. Vanuatu ina eneo lenye ukubwa wa zaidi ya kilomita mraba 12,000 na mji mkuu wake ni Port Vila.
Na katika siku kama ya leo miaka 412 iliyopita, Uholanzi ilianza kuikoloni kisiasa nchi ya Indonesia. Katika zama za wakoloni wa Kiholanzi nchini Indonesia, ardhi hiyo ilikuwa ikijulikana kwa jina la India ya Uholanzi na kabla ya hapo ilikuwa ikitawaliwa na kudhibitiwa na Wareno. Katika nusu ya pili ya karne ya 17 mkoloni Mholanzi alianza kuvidhibiti visiwa vya Indonesia na hatimaye kuidhibiti ardhi yote ya nchi hiyo. Hatimaye mwaka 1950 Indonesia ilijikomboa na kujitangazia uhuru wake chini ya uongozi wa Ahmad Sukarno.

0 comments:

Chapisha Maoni