Jumatano, Julai 30, 2014

MANENO YA ZITTO KABWE

Kwa kuwa tumeamua kupambana dhidi ya rushwa, hongo, ufisadi, uzembe na uvivu;
Kwa kuwa tumeamua kuhakikisha kuwa mali asili ya Nchi yetu Tanzania ni mali ya wananchi wote na kwamba lazima itumike kutokomeza umasikini nchini kwetu na kuleta maendeleo sawia na endelevu ya kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na kisiasa;
Kwa kuwa tumeamua kujenga Chama cha siasa chenye lengo la kuchochea ujenzi wa Taifa la Kujitegemea, lisilo na unyonyaji wala ubaguzi wa rangi, dini, kabila, jinsia, maumbile, hali ya kipato na lililo juu ya misingi ya haki kwa watu wake wote;
Kwa kuwa tumeamua kushiriki katika ujenzi wa Umoja wa Afrika ili kuwaenzi waasisi wa ukombozi wa Mwafrika na kujenga kontinenti lenye sauti yenye nguvu na ushawishi katika jamii ya mataifa ulimwenguni;
Kwa kuwa tumeamua kupigania demokrasia, uhuru wa mawazo, umoja, utu, uadilifu, uwajibikaji, uzalendo kwa Taifa na Amani;
Kwa kuwa kwa nia moja tumeamua kujenga chama cha mrengo wa kushoto chenye kufuata misingi ya Demokrasia ya Kijamii (Social Democracy), Demokrasia ya Rasilimali na misingi asili iliyoasisi Taifa letu (Unyerere) kama Azimio la Arusha[1]; na
Kwa wajibu tulio nao wa kujenga, kukuza na kuendeleza demokrasia na utamaduni wa mfumo wa vyama vingi Tanzania; Hivyo basi
[1] Tamko la Azimio la Arusha lililotolewa na Chama cha TANU mnamo mwezi Februari mwaka 1967 hususan Miiko ya Uongozi kama itakavyopfanyiwa marejeo mara kwa mara, pamoja na Maazimio mengine yatakayotangazwa na chama kwa mujibu wa Katiba hii yatakuwa ni marejeo halali ili kufikia maamuzi yeyote ya kisera ya Chama ..........

0 comments:

Chapisha Maoni