Beki was Aston Villa Ron Vlaar, 29, atakuwa na
mazungumzo na meneja wake Paul Lambert kuhusiana na hatma yake licha ya
Southampton kumwania (Daily Mirror), QPR wanafikiria kumchukua kiungo wa
Colombia Carlos Sanchez, 28, kwa pauni milioni 4 kutoka Elche (Daily
Mirror), West Ham na QPR wamepanda dau kwa Marseille kumchukua Matheiu
Valbuena baada ya kiungo huyo Mfaransa kukataa kuhamia Dynamo Moscow
(L'Equipe), Manchester United na Barcelona bado wanamfuatilia Juan
Cuadrado, 26, wa Fiorentina lakini huenda wakatishwa na bei ya pauni
milioni, 32, ya kiungo huyo kutoka Colombia (Marca), Manchester United
wamefikia makubaliano "ya mdomo" na kiungo wa Juventus Arturo Vidal, 27,
ya uhamisho wa pauni milioni 47 (Tuttosport), matumaini ya Manchester
City kumsajili beki kutoka Morocco Mehdi Benatia, 27, yamefifia baada ya
Roma kusema hakuna dalili za mchezaji huyo kuondoka (Le Figaro), meneja
mpya wa Manchester United amewaonya mashabiki wake kuwa timu hiyo
huenda ikasuasua katika miezi mitatu ya mwanzo wa msimu wakati wachezaji
wakianza kuzoea mbinu zake (Times), Van Gaal amesema iwapo watashinda
Ligi Kuu msimu ujao na kuwapiku majirani zao Manchester City, utakuwa
ushindi "mtamu" zaidi (Manchester Evening News), kiungo wa Manchester
City Yaya Toure, 31, amesema huenda akasalia katika timu hiyo hadi
atakapoacha kucheza soka (Guardian), mshambuliaji mpya wa Barcelona Luis
Suarez, 27, ambaye anatumikia adhabu ya miezi minne, amehamia katika
mji wa Pyrenees kuanza mazoezi ya msimu mpya akiwa na mwalimu binafsi
(Daily Mail), Didier Drogba, 36, amesema Diego Costa, 25, atakuwa
mchezaji "mkali" katika Ligi Kuu ya England (Sun), AC Milan wanafanya
mazungumzo wa mshambuliaji kutoka Brazil Robinho, 30 (Le Figaro), kiungo
wa Arsenal Santi Cazorla,29, bado anasakwa na Atlètico Madrid. Atlètico
pia wanamfuatilia Fernando Torres, 30, na winga wa PSV Eindhoven
Zakaria Bakkali, 18 (AS.com), kiungo anayefuatiliwa na Liverpool,
Xeridan Shaqiri, 22, huenda akaamua kubakia na klabu yake ya Bayern
Munich (Tuttosport), Borussia Dortmund na Schalke wanamtaka mshambuliaji
kutoka Serbia, Aden Ljajic, 22, kutoka AS Roma (Bild), Barcelona
wametangaza kumsajili kiungo kutoka Brazil, Alex Varoneze Dione
anayejulikana kama "Betri" kwa miaka mitatu (Mundodeportivo), Manchester
United wameanza tena kumfuatilia beki wa kati wa Atletico Madrid
Miranda, baada ya Atlètico kusema wapo tayari kupokea dau la pauni
milioni 23 (Metro), AC Milan wanamtaka winga wa Newcastle Hatem Ben Arfa
na huenda akauzwa kwa pauni milioni 12 (Daily Star), Bayern Munich wapo
tayari kusubiri hadi Oktoba kumsajili kipa wa zamani wa Barcelona
Victor Valdez ambaye anauguza jeraha la goti, ingawa anaweza kusita
kwenda kugombea namba na Manuel Neuer (Mundo Deportivo), QPR wanataka
kumchukua Ronaldinho ambaye amemaliza mkataba wake na Atletico Mineiro
(Globoesporte) na Chelsea wanakataa kutengeneza jezi zenye jina la kipa
Thibaut Courtois, 22 na Romelu Lukaku, 22, kwa sababu wachezaji hao bado
hawajapewa namba (Daily Star).
0 comments:
Chapisha Maoni