Kucha kwa wanawake ni eneo lingine linolatakiwa kuwekwa katika unadhifu.
Kuna baadhi ya wanawake unaweza kukutana nao kucha zao zimelika aidha
kwa kung'atwa au kwa kuliwa na fangasi.
Ipo aina fulani ya fangasi ya
kwenye kucha inawashamblia san wanawake hususan kwa mkoani Dar, sijui ni
kutokana na maji kwa sababu ya kufua au kuosha vyombo au kitu kingine.
Ni vyema wanawake wenye tatizo hilo kumuona tabibu mtaalamu wa ngozi kwa
msaada wa tiba. Unaweza kukutana na mwanamke kucha zake zimelika na
zina sharp edges kiasi kwamba akikugusa utadhani umeguswa na msasa.
Au
akishika Glasi ya Kinywaji ukiangalia kucha utadhani mkono ni wa
mwanaume maana kwa jinsi kucha zake zilivyo hata hafanani nazo. Kuna
kucha za bandia kama mwanamke ana matatizo ya kucha basi akazinunue
kusitiri aibu.
0 comments:
Chapisha Maoni