Kiungo wa Manchester United Marouane Fellaini huenda akaondoka kwenda
Napoli baada ya kufanya mazungumzo na mkuu wa klabu hiyo Riccardo Bigon
(Daily Express),United pia huenda wakamruhusu Shinji Kagawa, 25 kuondoka
huku Borussia Dortmund wakiwa tayari kumchukua tena (Independent),
Chelsea watalazimika kumuuza kipa Petr Cech, 32, kwenda PSG iwapo
watashindwa kumuuza Fernando Torres, 30, au John Obi Mikel, 27 (Daily
Telegraph), meneja wa Southampton Ronald Koeman
ana matumaini ya kumsajili kiungo Serge Gnabri, 19 na Carl Jenkinson,
22 kutoka Arsenal (Daily Star), hata hivyo Southampton wanakabiliwa na
ushindani mkali kutoka kwa West Ham wanaokaribia kumchukua Jenkinson kwa
mkopo (Daily Mirror), beki wa kulia wa Sporting Lisbon Miguel Lopez, 27
anajiandaa kujiunga na Tottenham kwa mkopo, huku akitazamia uhamisho wa
kudumu baadaye (Daily Mail), meneja wa Liverpool Brendan Rodgers
amethibitisha kuwa hawatopanda dau tena kumchukua Loic Remy (Daily
Mirror), lakini Newcastle United huenda wakajaribu kumchukua tena Remy
kwa mkopo (Goal.com) meneja wa Aston Villa Paul Lambert anataka
kumsajili Victor Moses, 23, kwa mkopo na pia kumchukua Ki Sung-yeung, 25
kutoka Swansea wiki hii (Daily Telegraph), wakala wa Samuel Eto'o
amewaambia West Ham kuwa mchezaji huyo yuko huru kujiunga nao, kuziba
pengo la Andy Carroll aliyeumua, lakini Eto'o anataka mshahara wa pauni
100,000 kwa wiki (Daily Mail), mkurugenzi mkuu wa Juventus Beppe Marotta
amesema klabu yake itajitahidi kutomwachilia Arturo Vidal, na kutupilia
mbali taarifa kuwa mchezaji huyo anakwenda Chelsea (Tottosport),
Southampton wanafikiria kumchukua beki wa kati wa Sporting Lisbon Marcos
Rojo, 24, kufutia kuondoka kwa wachezaji wengi Saints (Le Figaro),
Atletico Mineiro amethibitisha kuondoka kwa kiungo wa zamani wa
Barcelona Ronaldinho, 34 (L'Equipe), mshambuliaji wa Ubelgiji Divock
Origi, 19, amesaini mkataba wa miaka mitano na Liverpool (Bild), PSG
wameruhusu mshambuliaji wao Ezequiel Lavezzi, 29, kwenda Atletico
Madrid. Mchezaji huyo anasakwa pia na Liverpool (AS.com) Lazio ya Italia
imetangaza kuwa inamchukua beki wa Feyenoord Stefan de Vrij, 22
(L'Equipe)
0 comments:
Chapisha Maoni