Mazoezi ni muhimu kwa mwanadamu kwa ajili ya kuuweka mwili katika hali
nzuri kiafya, lakini wengi wetu tumekuwa wavivu sana kufanya mazoezi
hata ya kutembea. Kwa upande wa wanawake wa hapa nchini hili ni tatizo
kubwa. Wanawake wengi hapa nchini ni wavivu katika kufanya mazoezi na
ndio sababu wengi wana vitambi na hivyo watu wengi kudhani kwamba wana
ujauzito.
Urembo kwa mwanamke unajumuishwa na muonekanao wa mwili kama umekaa
katika shepu nzuri. Sura siyo hoja sana, bali maumbile. kuna baadhi ya
wanawake wamejaaliwa kuwa na sura na maumbo mazuri lakini baada ya
kufakamia bia na nyama choma hususan kiti moto huumuka na kuwa na maumbo
makubwa na mabaya yasiyo na mvuto.
Mazoezi hayahitaji gharama, maana wengi hapa watakuja kulalamika kwamba hawana fedha za kwenda Gym.
Mazoezi hayahitaji gharama, maana wengi hapa watakuja kulalamika kwamba hawana fedha za kwenda Gym.
0 comments:
Chapisha Maoni