Jumatatu, Julai 07, 2014

KINARA WA REAL MADRID AMEFARIKI DUNIA

Mchezaji nguli wa Real Madrid Alfredo Di Stefano, anayetajwa kuwa mmoja wa wachezaji wazuri duniani amefariki dunia.
Mchezaji huyo wa zamani wa Real Madrid aliyekuwa na umri wa miaka 88 alipatwa na mshtuko wa moyo siku ya Jumamosi na kulazwa katika hospitali ya Gregorio Maranon mjini Madrid.
Real Madrid imethibitisha taarifa hizo, ikisema Di Stefano ambaye ni Rais wao wa heshima amefariki dunia.
Katika uhai wake alishinda makombe matano ya Ulaya, akifunga katika kila mchezo wa fainali kati ya mwaka 1956 na 1960.
Rais wa Real Madrid, Florentino Perez amesema bodi ya klabu 'imesikitishwa na kupeleka rambirambi kwa watoto, familia na marafiki'.
Alizaliwa nchini Argentina, lakini mafanikio yake aliyapata Ulaya kwa kuweza kushinda vikombe vinane vya ligi kuu ya Spain, na kuwa mchezaji bora wa mwaka wa Ulaya mwaka 1957 na 1959.

0 comments:

Chapisha Maoni